Mshambuliaji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Heritier Makambo amejiunga tena Yanga sc kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru akitokea klabu ya Horoya ya Guinea.
Mpachika mabao huyo aliyewahi kuwika Jangwani na kuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo alitimkia nchini Guinea mwaka 2019 kujiunga na Horoya baada ya kuifungia Yanga mabao 17.
Makambo anatajwa kuchukua nafasi ya Mghana Michael Sarpong anayehusishwa kutemwa na mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania baada ya jezi yake namba 19 kupewa Makambo.
Yanga kwa kwasasa imeshasajili mastraika wawili Makambo na Mayele. kuboresha safu ya ushambuliaji iliyoonekana kusuasua msimu uliopita.