Home Soka Man United Yatua Top 3

Man United Yatua Top 3

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kutua nafasi ya tatu katika msimamo ligi kuu nchini Uingereza baada ya kutoa sare na Westham United katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.

Paul Pogba aliunawa mpira mwishoni mwa kipindi cha kwanza na mwamuzi baada ya kuangalia marudio ya refa wa video aliamuru penati ambayo ilifungwa na Antonio na baada ya kutoka mapumziko iliwachukua Man United dakika 6 kusawazisha bao hilo kupitia kwa Mason Greenwood kufuatia kupasiana vizuri ndani ya box.

Kutokana na msimamo ulivyo Man United imepanda mpaka nafasi ya tatu ikiwa na alama 63 huku itaivaa Leicester City katika mchezo wa mwisho ambapo itahitaji alama moja tu kufuzu kucheza michuano ya klabu bingwa ulaya msimu ujao.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited