Bosi mpya wa klabu ya Simba sc Senzo Masingizi ameoneshwa kufurahishwa na kazi ya Afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara kuhamasisha mashabiki wa timu hiyo kujaa uwanjani na kuipenda timu yao.
Bosi huyo raia wa Afrika Kusini ambaye ametambulishwa leo mbele ya waandishi wa habari ameonesha kumkubali manara baada ya kumkabidhi kazi ya kuhamasisha mashabiki wa timu hiyo.
“Nimekua nikimfatilia Haji manara,mambo anayofanya kwenye vyombo vya habari ndivyo inavyotakiwa,wahamasishe mashabiki wa simba wajae uwanjani na waipende timu yao”.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kauli hiyo ya bosi mpya imeonesha kujibu maswali ya wadau wengi wa michezo kuhusu hatma ya Manara klabuni hapo baada ya hivi karibuni klabu hiyo kutangaza nafasi za kazi ikiwemo ya Afisa habari ambayo ilikua ikishikiliwa na manara.