Home Soka Manji Ashikiliwa Takukuru

Manji Ashikiliwa Takukuru

by Dennis Msotwa
0 comments

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imethibitisha kuwa inamshikilia mfanyabishara Yusuf Manji kwa mahojiano kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi Salum Hamdun amesema kuwa Manji ambaye amerejea nchini baada ya kuondoka tangu mwaka 2018 anatuhumiwa kwa makosa matatu.

CP Hamdun amesema tuhuma hizo zinahusisha kampuni zake za Intertrade Commercial Ltd Serivice na Golden Globe International Service Limited.

banner

Tuhuma ya kwanza ni kuisababishia serikali hasara kwa kukwepa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na udanganyifu wakati akifanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Pili, inadaiwa kuwa kupitia kampuni ya Golden Globe alifanya udanganyifu wakati wa kununua hisa za kampuni ya mawasiliano ya Tigo.

Tatu ni tuhuma ya mapato ya Yanga SC yanayohusu kampuni ya Quality Group.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited