Beki wa kushoto wa Ruvu Shooting Edward Charles Manyama jana jioni amemalizana na Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC kwa kusaini kandarasi ya miaka miwili (2) kwa mujibu wa taarifa za ndani za klabu hiyo.
Manyama amekuwa na kiwango bora tangu msimu uliopita na kupata nafasi kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) huku akishtua wadau wa michezo baada ya kuhama kutoka katika klabu ya Namungo Fc inayoshiriki michuano ya kimataifa na kwenda Jkt Tanzania kwa mkataba wa miezi 6.
Tayari mchezaji huyo alishahusishwa na Yanga sc huku taarifa zikidai kuwa alishamalizana na Yanga sc na ilibaki kusaini tu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.