Home Soka Matajiri Newcastle wawekewa vikwazo na vilabu EPL

Matajiri Newcastle wawekewa vikwazo na vilabu EPL

by Dennis Msotwa
0 comments

Vilabu vinavyoshiriki ligi kuu soka nchini Uingereza vimepiga kura ya kuweka kizuia kwa klabu kuingia mikataba ya kibiashara na makampuni ya tajiri anayevimiliki moja kwa moja.

Hilo limekuja kama tahadhari kutokana kuripotiwa kuwa Newcastle United ipo kwenye mipango ya kuingia makubaliano ya kibiashara na makampuni yanayomilikiwa na Bilionea Mwana Mfalme wa Saudi Arabia Mohamed Bin Salman ambaye ndiye mmiliki mpya wa klabu hiyo,

banner

Hatua hiyo ingeiwezesha klabu hiyo kuingiza pesa nyingi kwa muda mfupi hali mabayo ingesababisha fujo kwenye soko la usajili na hiyvyo kwenda kinyume na sheria za matumizi ya fedha yaani FIFA Financial Fair play(FFF).

Tangu kununuliwa kwa timu hiyo na matajiri hao kutoka Saudi Arabia kumekuwa na wasiwasi juu ya matumizi ya fedha kutokana na Bin Salman kuwa ndiye mmiliki tajiri zaidi wa klabu duniani.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited