Baada ya kumkosa kocha wao kipenzi Ettiene Ndayiragije ambae taarifa zinadai amemalizana na Azam Fc timu ya Kmc imeamua kumpa mkataba kocha Selemani Matola ili kuziba nafasi ya Mrundi huyo ambae ameifundisha Kmc kwa mafanikio makubwa na kuifanya kushika nafasi ya nne ya ligi kuu Tanzania bara na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.
Matola anayeifundisha Lipuli fc ya Iringa ameifanya timu hiyo kuwa tishio kwa vigogo wa soka nchini Simba na Yanga hasa inapocheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Samora uliopo mkoani humo.Licha ya ushindani alitoa katika ligi kuu pia ameiwezesha timu hiyo kufika fainali ya michuano ya kombe la shirikisho ambapo walipoteza dhidi ya Azam Fc.
Imeripotiwa mazungumzo kati ya wanakinondoni hao na Matola yapo katika hatua nzuri na anaweza kupewa mkataba muda wowote kuchukua nafasi hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.