Klabu ya Mbao Fc ya jijini Mwanza imeendelea kupata ushindi baada ya kuifunga Namungo Fc mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa jijini Mwanza.
Mabao ya Mbao Fc yalifungwa mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa Jordan John dakika ya 4 na 14 huku Abdulkareem Segeja akifunga bao la tatu dakika ya 28 na kuipa Mbao Fc ushindi wa saba mfululizo na kuelekea kuepuka kushuka daraja.
Mbao imeendeleza matokeo ya ushindi chini ya kocha Fred Felix Minziro ambaye aliletwa ili kuinusuru timu hiyo isishuke daraja ambapo sasa imefikisha alama 42 nafasi ya 16 ya msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.