Mshambuliaji Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa upande wa wanaume akiwabwaga Cristiano Ronaldo na beki wa Liverpool Virgil Van Dijk katika tuzo zilizotolewa usiku huu jijini Milan.
Awali ilidhaniwa beki Van Dijk atachukua tuzo hiyo baada ya kuwa ametwaa ile ya mchezaji bora barani ulaya baada ya kuisadia liverpool kuchukua taji la klabu bingwa barani ulaya.
Hiyo ni mara ya sita kwa staa huyo wa Barcelona akimbwaga hasimu wake Ronaldo aliyechukua tuzo hiyo mara tano akimrithi Luka Modric aliyeshinda tuzo hiyo mwaka jana.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pia kocha Jurgen Klopp alichukua tuzo ya kocha bora huku kipa Alison Becker pia wa Liverpool alichukua tuzo ya kipa bora.