Wachezaji wa Yanga Metacha Mnata na Abdulaziz Makame ‘Bui’ wamesajiliwa na kampuni ya AfriSoccer ambayo inahusika na uwakala wa kuwatafutia wachezaji timu nje ya nchi ili wapate nafasi ya kucheza za ulaya.
Kampuni hiyo imewasajili Metacha na Bui baada ya kuvutiwa na uwezo wa Nyota hao ambao pia wako timu ya Taifa, watakuwa na nafasi ya kujaribu bahati yao nje ya nchi kama zitatokea timu kuwahitaji
Hata hivyo kwa sasa wana mikataba na Yanga, ikitokea timu kuwahitaji, italazimika kumalizana na Yanga kwanza kitu ambacho kinaweza kuleta ugumu kwani timu nyingi za nje hupenda wachezaji waliomaliza mikataba ili kuepuka gharama.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.