Kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime anatajwa kutua jangwani muda wowote kumsaidia Bonifasi Mkwasa baada ya timu hiyo kuvunja benchi la ufundi lililokua likiongozwa na Mwinyi Zahera na Noel Mwandila.
Kocha aliyeifundisha Mtibwa Sugar kabla ya kutua Kagera amekua kwenye mazungumzo na Yanga na inadaiwa muda wowote anaweza kutua klabuni hapo kujiunga na Mkwasa.
Tangu timu hiyo ivunje benchi la ufundi Mkwasa amekua akisaidiwa na Said Maulid ambaye ni kocha wa kikosi B cha klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mexime amekua na mafanikio msimu huu akiwa na Kagera ambapo ameingoza timu hiyo kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.