Mshambuliaji wa Yanga David Molinga ameiokoa timu hiyo na kipigo baada ya kufunga mabao mawili ya kusawazisha kufuatia kufunga mabao 3-1 mpaka dakika ya 58 ya mchezo dhidi ya Polisi Tanzania uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Yanga walianza kupachika bao la uongozi dakika ya 6 kupitia kwa Mrisho Ngasa aliyemalizia krosi ya Juma Abdul bao lililodumu mpaka dakika ya 35 ambapo Ditram Nchimbi alisawazisha bao hilo na kufunga mengine mawili dakika za 55’na 58′.
Molinga alisaawazisha mabao hayo dakika ya 65 baada ya kumalizia mpira ulioshindwa kuokolewa na kipa wa Polisi na kisha dakika ya 69 alifunga tena kwa kiki ya faulo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga leo ilimkosa kocha Mwinyi Zahera ambaye ameanza kutumikia adhabu ya kukosa mechi tatu baada ya kutovaa nadhifu katika mechi dhidi ya Ruvu shooting ambayo yanga ilipoteza pamoja na kutoa lugha isiyo na staha kwa shirikisho na soka nchini pamoja na bodi ya ligi kuu.