Home Soka Morocco “Out” Afcon 2024

Morocco “Out” Afcon 2024

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Taifa ya Morocco imetolewa katika michuano ya mataifa ya Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa timu ya Taifa ya Afrika Kusini katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Kinyume na matarajio ya wengi Morocco iliyosheheni mastaa wakubwa barani ulaya licha ya kumiliki mpira kwa kiwango cha juu ilikubali kipigo hicho dakika ya 57 baada ya Evidence Makgopa kuandika bao la kwanza baada ya kujitega sehemu sahihi na kupokea pasi nzuri kutoka kwa Mokoena.

Morocco waliamua kushambulia moja kwa moja na kuathiri umbo lao la ulinzi hali iliyokaribisha mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwao na kupelekea Afrika kusini kupata faulo iliyofungwa kiufundi Teboho Mokoena dakika ya 95 ya mchezo huku kiungo Sofyan Amrabat akipata kadi nyekundu.

banner

Sasa Afrika Kusini baada ya kufuzu hatua ya nusu fainali itakutana na Cape Verde ambayo ilifanikiwa kuifunga Mauritania katika mchezo wa hatua ya robo fainali.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited