Home Soka Morrison,Yanga Wavimbiana

Morrison,Yanga Wavimbiana

by Sports Leo
0 comments

Nyota wa Klabu ya Yanga, Benard Morisson ameamua kurudisha fedha dola 30,000 (zaidi ya Milioni 60 za Kitanzania) kutoka Yanga ambazo zilikuwa fedha za usajili wa mkataba mpya wa miaka miwili.
Yanga walikuwa wamekubaliana kila kitu na Morisson kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la dola 50,000 na mshahara wa dola 5,000 Ila nyota huyo alikuwa hajapewa fedha hizo.
Baada ya sintofahamu kuhusu mkataba mpya wa Morisson na Yanga. Viongozi wa Yanga waliamua kumuwekea nyota huyo dola elfu 30,000 kwenye akaunti yake ikiwa ni fedha za kusaini mkataba mpya wa miaka miwili Kitu ambacho Morrison amewaambia watu wa benki wazirudishe fedha hizo kwa watu waliotuma (Yanga) kwani yeye hazitambui.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited