50
Inaelezwa kuwa Noureddine Al-Nabi aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya El-Merreikh kabla ya kuondoshwa, amefanikiwa kuwa Mkuu wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam walio Mabingwa wa Kihistoria wa Nchi.
Mabosi wa Yanga hawaridhishwi na kiwango ambacho timu yao imekuwa ikikionyesha hata baada ya Kaze kuondoka.
Taarifa za ndani zinasema Mabosi na kocha wameshakubaliana kilakitu na Nabi atawasili na msaidizi wake hivyo kibarua cha Juma Mwambusi kiko matatani.
Huenda akatambulishwa kabla ya mechi dhidi ya Azam ya Jumapili tarehe 25.04.2021.
Endapo kocha huyu atafanikiwa kuanza kazi kwa Yanga atakuwa ni kocha wa nne msimu kuwafundisha mabingwa hao wa kihistoria.