Kocha wa timu ya Mbeya city Juma Mwambusi amewasilisha barua ya kujiuzuru kazi ya kuifundisha timu hiyo baada ya kuwa na mwenendo usioridhisha.
Mwambusi aliyewahi kuifundisha timu hiyo kwa mafanikio kabla ya kuondoka na kujiunga na Yanga kisha Azam akiwa kocha msaidizi wa Hans van Pluijm kabla ya kuondoka na kurudi Mbeya city.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, James Kasusura imeeleza kuwa Kocha Mwambusi aliwasilisha barua ya kuomba kujiuzulu mnamo tarehe 26/11/2019 kwa maslahi mapana ya timu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.