Sasa rasmi klabu ya Yanga sc imeachana na kocha msaidizi Juma Mwambusi kwa sababu zilizoelezwa za kiafya ambazo zimethibitishwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo Dk.Mshindo Msolla.
Hii ni mara ya pili kwa Mwambusi kuondoka klabuni hapo ambapo awali aliondoka pamoja na aliyekua kocha wa zamani Hans Van Plujm waliyeibukia tena pamoja katika klabu ya Azam Fc.
Bado mpaka sasa haijajulikana kama kocha huyo ameondoka kwa sababu zingine ama ni kwa matatizo ya afya kama ilivyoripotiwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.