Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika, Namungo FC wanaondoka nchini leo kuelekea Angola kuwafuata wenyeji wao CD Primeiro De Agosto bila nyota wake wanne wa kikosi cha kwanza.
CD Primeiro De Agosto itaikaribisha Namungo katika mechi ya kwanza ya hatua ya mtoano itakayochezwa keshokutwa nchini humo.
Nyota hao ambao wameachwa katika msafara wa timu hiyo ni pamoja na Blaise Bigirimana, Abdulhalim Humud, Amani Kiata na Adam Salamba.
Katibu Mkuu wa Namugo FC, Ally Suleiman, alisema kikosi cha timu hiyo kimeondoka na wachezaji 23 na baadhi ya nyota walioachwa inatokana na kuwa majeruhi pamoja na matatizo ya kifamilia.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Suleiman alisema Humud na Amani Kiata wamelazimika kubaki kwa sababu ya matatizo ya kifamilia wakati Bigirimana ni majeruhi huku Salamba akiwa kwenye mchakato wa kuondoka kuelekea Serbia ambako ameuzwa.
Cc:Michezoonline