Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Singida Fountain Gate Fc Meddie kagere amejiunga na klabu ya Namungo yenye maskani yake mkoani Mtwara katika wilaya ya Ruangwa kwa mkataba wa mkopo wa miezi 6.
Mchezaji huyo wa zamani wa Simba sc alijiunga na Singida Fountain Gate mwaka ambapo baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa nusu msimu sasa amejiunga na Namungo Fc kumalizia sehemu ya pili ya msimu huu wa ligi kuu na Nbc.
Pia klabu hiyo imemsajili Aliyewahi kuwa kiungo Vilabu vya Coastal Union na Mbeya City Fc Ayoub Semtawa kwa mkataba ambao haukuwekwa wazi na mabosi wa klabu hiyo yenye mashabiki wengi katika mikoa ya kusini mwa Tanzania.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc ambayo mpaka sasa imesimamishwa Namungo Fc inashika nafasi ya nane ikiwa na alama 17 ikiwa imecheza jumla ya michezo 14 mpaka sasa ambapo usajili wa Kagere unakwenda kuziba pengo la mshambuliaji Reliants Lusajo ambaye amejiunga na Mashujaa Fc.