Baada ya kununuliwa na familia ya kifalme ya Saudi Arabia chini ya mwana mfalme Bin Sueiman klabu ya soka ya Newcastle United ya Uingereza imeanza mipango kabambe ya usajili kuanza kuisuka timu hiyo kuwa ya ushindani zaidi kwenye ligi kuu ya soka nchini Uingereza.
Klabu hiyo imwewaka kwenye rada zao wachezaji wanne wa Manchester United beki Eric Baily aliepoteza namba baada ya ujio wa Rafael Varane kutoka Real Madrid,viungo Jesse Lingard na Don Van De Beek ambao wamekosa dakika za kutosha uwanjani pamoja na mshambuliaji Anthony Martial anayesugua benchi kwasasa.
Timu hiyo pia ipo kwenye mipango ya kumuajiri Ralph Rangnick kuwa Mkurugenzi mpya wa michezo wa klabu hiyo kusuka idara ya usajili lutokana na uzoefu wake kufanya kazi RB Leipzig ya Ujerumani.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mabosi wa timu hiyo wapo kwenye mipango ya kumtimua kocha mkuu wa timu hiyo Steve Bruce huku makocha Antonio Conte,Steven Gerrard na brendan Rodgers wakiwa kwenye mipango yao.