Mshambualiaji wa Brazil Neymar Jr ataikosa michuano ya kombe la shirikisho barani America maarufu kama Kopa Amerika baada ya kuumia kifundo cha mguu wake wa kulia katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na michuano hiyo dhidi ya Qatar hapo jana.
Staa huyo anaichezea klabu ya Psg ya nchini Ufaransa aliumia dakika 20 za mwanzo wa mchezo baada ya staa wa Everton Richalson kuifungia Brazil bao la kwanza kwa kichwa na wakati wachezaji wenzie wakiungana kushangilia,Neymar alionekana akielekea vyumbani na timu ya madaktari kwa ajili ya matibabu na baadae aliondoka kabisa uwanjani hapo.
Nyota huyo hakuwa na msimu mzuri baada ya hivi karibuni kukosa mechi za 13 klabu yake sababu ya majeraha,Pia wiki iliyopita alitolewa unahodha wa timu ya taifa na nafasi yake alichukuliwa na mkongwe Dani Alves.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Katika taarifa iliyotolewa na chama cha soka cha Brazil inasema mchezaji huyo atakosa michuano hiyo baada ya vipimo kuonesha amepata matatizo katika kifundo cha mguu hivyo hataweza kushiriki michuano hiyo huku benchi la ufundi la timu ya taifa litatafuta mchezaji atakayeziba nafasi ya staa huyo.