Home Soka Neymar:Kombe la dunia 2022 ni la mwisho kwangu

Neymar:Kombe la dunia 2022 ni la mwisho kwangu

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Brazil Neymar Jr ameweka wazi kuwa anadhani kombe la dunia 2022 nchini Qatar ndio litakuwa la mwisho kushiriki kwake kwani haoni kama ana nguvu na akili ya kujihusisha na soka kwa muda mrefu.

Neymar ambaye anakimbizia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Taifa hilo alianza kulitumikia Taifa hilo mwaka 2010 huku ubingwa pekee alioshinda na Brazil ni ule wa kombe la Mabara 2013.

Akiongea na gazeti la The Athletic alisema ”nafikiri litakuwa kombe la dunia la mwisho kushiriki,nadhani itakuwa hivyo kwasababu sidhani kama akili yangu na nguvu viko tayari kudili na soka tena”.

banner

Aliendelea ”nitajitahidi kujitoa na kufanya kila kitu kwaajili ya timu yangu na wachezaji wenzangu na naamini naweza kutimiza ndoto yangu ya tangu utotoni kutwaa kombe la dunia”.

Neymar mwenye miaka 29 amekuwa akilaumiwa na Wabrazil kuwa hajitumi vya kutosha kuipa mataji Brazil tofauti na kipaji chake kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake Ronaldo,Ronaldinho na wengineo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited