Home Soka Ni Simba,Yanga,Azam nusu fainali Mapinduzi

Ni Simba,Yanga,Azam nusu fainali Mapinduzi

by Sports Leo
0 comments

Miamba mitatu ya soka nchini Tanzania vilabu vya Simba,Yanga na Azam vimefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea huko visiwani Zanzibar.

Azam walio kundi A wana alama 6 baada ya michezo miwili baada ya jana kuifunga Namungo na kujikatia tiketi hiyo kutokana na kuongoza kundi lao.

Yanga wao baada ya sare ya 2-2 dhidi ya mabingwa wa Zanzibar KMKM wamefikia alama nne na kuongoza kundi B hivyo kujikatia tiketi muhimu ya hatua inayofuata.Ikumbukwe katika mchezo wa awali walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Taifa Jang’ombe.

banner

Nao mabingwa watetezi wamefuzu hatua hiyo ya nusu fainali kutokana kujikusanyia alama nne baada ya michezo miwili.Mchezo uliomalizika hivi punde wametoka sare ya bila kufungana na Mlandege.

Utamu wa michuano umeongezeka baada ya timu hizo kufuzu,huku mbili kati ya hizo ni lazima zitakutana katika hatua ya nusu fainali,hata hivyo wadau wa soka visiwani Zanzibar wanatamani kuziona klabu zao pendwa Simba na Yanga katika hatua ya fainali.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited