Klabu ya Simba sc imeanza kutafuta mbadala wa wachezaji Cletous Chama na Jonas Mkude kufuatia wachezaji hao kuonyesha nidhamu mbovu katika kikosi hicho.
Katika kuonyesha kuwa wako siriazi na suala la nidhamu tayari mabosi wa timu hiyo wameanza kumfukuzia kiungo mkenya anayecheza kunako klabu ya Zesco United ya Zambia Antony Teddy maarufu kama “Akumu”.
Kiungo huyo mwenye uwezo wa kukaba na kushambulia anamaliza mkataba wake mwezi desemba na tayari mabosi hao wameshaanza mawasiliano na wakala wa mchezaji huyo ambaye huwaletea mastaa klabuni hapo ili kusajili kiungo wakati wa dirisha dogo litakalofunguliwa hivi karibuni na kufungwa desemba.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mtendaji mkuu wa Simba amesikika akidhibitisha kufanya usajili wa kiungo huyo japo lengo kuu la klabu ni kusajili mshambuliaji atakayesaidiana na Kagere baada ya John Boko kupata majeraha na Wilker kushindwa kuonesha kiwango.