Home Soka Ninja Aanza Kazi Gallax

Ninja Aanza Kazi Gallax

by Sports Leo
0 comments

Beki wa zamani wa Yanga sc Abdallah Shaibu “Ninja” ameanza kucheza katika timu ya L.A gallax baada ya jana kucheza mechi ya kwanza ya kikosi cha pili cha timu hiyo dhidi ya New mexico.

Ninja katika mchezo huo licha kucheza vyema alisababisha penati dakika ya 76 ya mchezo hali iliyowapa New mexico goli la kusawazisha na mchezo kumalizika kwa sare ya mabao 2.

Beki huyo mrefu aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Nicholas DePuy lakini kutokana na ugeni alishindwa kuendana na kasi ya mchezo baada ya kushindwa kuokoa mpira ndani ya boxi hali iliyomfanya acheze faulo kumzuia mshambuliaji wa New mexico asifunge hali ilimlazimu mwamuzi kutoa adhabu ya penati.

banner

Awali, Ninja alisaini miaka minne na klabu ya Ligi Daraja la Tatu ya Jamhuri ya Czech na kisha kupelekwa kwa mkopo katika klabu ya LA Galaxy ya nchini Marekani ambako atacheza kwa msimu mzima.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited