Aliyekuwa mlinzi wa Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amerejea visiwani Zanzibar baada ya klabu ya LA Galaxy kusitisha mkataba wake imefahamika
Aidha Wakala wa mchezaji huyo amesema pia klabu ya MFK Karvina ya Jamhuri ya Czech ambayo ndio ilimsajili Ninja na baadae kumtoa kwa mkopo LA Galaxy, nayo imesitisha mkataba wake bila kutoa sababu zozote
Ninja alirejea nchini baada ya ligi kuu ya Marekani kumalizika na alitakiwa kurudi huko Marekani mwezi huu
Inaelezwa kwa sasa anafuatilia kibali cha kurudi Ulaya kwenda kufanya majaribio katika timu nyingine ambazo zimeonyesha kuhitaji huduma yake
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ninja aliitumikia klabu ya Yanga kwa misimu miwili kabla ya kugoma kuongeza mkataba mwezi Julai baada ya kupata ofa ya kujiunga na MFK Karvina