Mwenyekiti wa klabu ya Simba sc Swedi Nkwabi amejiuzuru nafasi yake ya Mwenyekiti wa klabu hiyo kuanzia leo baada ya kutumikia nafasi hiyo kwa muda tangu timu hiyo ilipofanya mabadiliko ya uendeshaji.
Katika barua ambayo Swedi ameiandikia Bodi ya Wakurugenzi kupitia Mwenyekiti wa Bodi amesema sababu kuu ya kijiuzuru nafasi hiyo ni kuhitaji muda zaidi kusimamia shughuli zake binafsi ambazo hakuziweka wazi.
Aidha taarifa hiyo iliyotolewa na klabu hiyo kupitia kwa bodi ya Wakurugenzi na Sekretarieti ya Simba inamtakia kila la heri katika shughuli zake, huku ikitumaini kwamba ataendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za klabu kama ilivyokuwa awali kabla kupata nafasi hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pia klabu hiyo imetangaza kuwa utaratibu wa kumpata Mwenyekiti mpya utatangazwa hapo baadae,Huku kukiwa na sintofahamu kuhusu suala hilo maana ni takribani wiki moja toka aliyekua afisa mtendaji mkuu Crentious Magori kuachia ngazi akimpisha Senzo Mazingizi.