Home Soka No Deal!

No Deal!

by Sports Leo
0 comments

Imeripotiwa kwamba ule mpango wa klabu ya Manchester United kumsajili kiungo wa Ureno na klabu ya Sporting Lisbon Bruno Fernandez umekufa rasmi baada ya klabu hizo kushindwa kufikia makubaliano.

Chanzo cha dili hilo kufa ni kutokana na klabu hizo kumthaminisha tofauti mchezaji huyo huku Sporting wakihitaji takribani paundi milioni 68 kumuachia mchezaji huyo na United wakiwa tayari kulipa fedha hizo kwa awamu kulingana na uwezo wa mchezaji atakaounyesha klabuni hapo.

Kufa kwa dili hili kunatajwa kutazidisha presha kwa wamiliki wa klabu hiyo ambapo mashabiki wa klabu hiyo wamechoshwa na sera za uendeshaji wa klabu hivyo kuhitaji mabadiliko hasa kwa upande wa utawala.

banner

Inasemekana mashabiki nchini humo wamejipanga  kutembea kwa dakika 58 katika mechi dhidi ya Wolves ili kuwakumbuka wenzao waliofariki katika ajali ya ndege mwaka 1958 pia wakishinikiza klabu hiyo kubadili umiliki kutoka kwa wamarekana Glazer ambao wameegemea kupata faida kupitia biashara huku timu ikizidi kudidimia uwanjani.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited