Aliyekua kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Augustine Okrah anatajwa kumalizana na Yanga sc kuja kuongeza nguvu katika usajili wa dirisha dogo la mwezi huu ikiwa ni mapendekezo ya kocha Miguel Gamondi wa klabu hiyo.
Taarifa za ndani zaidi zinasema kuwa tayari nyota huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kujiunga na klabu hiyo na anatarajiwa kutambulishwa rasmi Disemba 31 siku ya mchezo wa ufunguzi wa klabu hiyo wa michuano ya mapinduzi visiwani Zanzibar.
Okrah alitemwa na Simba Sc mwishoni mwa msimu uliopita akitajwa kuwa mtovu na nidhamu na alirejea nchini Ghana na kujiunga na klabu ya Benchem United ambapo amekua na kiwango bora zaidi kiasi cha kuwashawishi mabosi wa Yanga sc kumrudisha nchini.
Inatajwa kuwa usajili wa kiungo huyo wa pembeni ni pendekezo la kocha Miguel Gamondi na anakuja kuchukua nafasi ya Jesus Moloko ambaye kwa mujibu wa kocha Gamondi ameona haingii vyema katika mfumo wake anaotaka kuutumia kutokea pembeni ya uwanja.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Okrah tangu ajiunge na Benchem United msimu huu tayari amefunga jumla ya magoli nane na kutoa assisti mbili katika michezo 15 ya ligi kuu nchini humo huku akitajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba mwaka huu.