Klabu ya Yanga ipo katika hatua za mwisho kumsajili kiungo Ally Niyonzima kutoka klabu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda.
Niyonzima 24 ni kiungo wa nafasi ya ulinzi ambayo inachezwa na Papy Tshitshimbi hivyo anakuja kuwa msaada kwa kiungo huyo kwa mujibu wa kocha wa Yanga Luc Eymael.
Mchakato wa kumsajili kiungo huyo unafanywa na wadhamini wa klabu hiyo Gsm ambapo usajili huo ni kukamilisha mapendekezo ya mwalimu Luc Eymael ambaye amidhinisha usajili huo.\
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kiungo huyo ana uzoefu na mechi za kimatafa akiwa ameshirika michuano ya Afcon na ligi za kimataifa za Caf pia aliicheza soka la kimataifa katika klabu ya Al Bashaer nchini Oman.