Viungo wa Manchester United Paul Pogba na Bruno Fernandes wameiongoza timu yao kuichakaza Leeds United magoli 5-1 katika mchezo wa ligi kuu ya England uliopigwa Old Trafford.
Bruno Fernandes aliondoka na mpira baada ya kufunga magoli matatu(hat-trick) ikiwa ni ya kwanza kwake tangu ajiunge na timu hiyo na anakuwa mchezaji wa 10 kwenye historia ya ligi hiyo kufunga hat-trick katika mchezo wa ufunguzi.
Kwa upande wa Paul Pogba ameandikiwa pasi nne za usaidizi kwa timu yake akiwa ni mchezaji wa saba kwenye historia ya ligi hiyo kutoa idadi hizo za pasi za mwisho na kuiwezesha Man Utd kukaa kileleni mwa ligi hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.