Taarifa mbaya ni kuhusu kupata ajali kwa kikosi cha timu ya Polisi Tanzania waliokuwa wakitoka mazoezini asubuhi ya leo huku ikidaiwa kwamba baadhi ya mastaa wa kikosi hicho wamepata majeraha makubwa.
Taarifa zaidi zinadai kuwa kikosi hicho kilichopata ajali kinajumuisha wachezaji,viongozi wa benchi la ufundi na viongozi wa timu kadhaa huku ikisemekana hali ya mchezaji Gerrad Mdamu ikiwa sio nzuri kiasi cha kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Kcmx mjini Moshi.
”Timu yetu ya Polisi Tanzania imepata ajali asubuhi ya leo tukitoka mazoezini, wachezaji waliopata majeruhi 13, dereva na mwalimu Msaidizi. Mchezaji Gerald Mdamu hali yake si nzuri na wote wamelazwa KCMC wakindelea na matibabu”.Ilisomeka taarifa kutoka katika moja ya mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.