Home Soka Ronaldo atupia mbili Utd ikiiua Newcastle

Ronaldo atupia mbili Utd ikiiua Newcastle

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji mpya wa mashetani wekundu Cristiano Ronaldo ameweka kambani magoli mawili kwa timu ya Manchester United katika ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Newcastle United kwenye mchezo wa wa ligi kuu ya Uingereza uliofanyika hii leo katika dimba la Old Trafford jijini Manchester.

Ronaldo aliweka goli la kwanza kunako dakika ya 45+2 ya kipindi cha kwanza akimalizia mpira uliomshinda golikipa wa Newcastle Woodman baada ya shuti kali la Mason Greenwood.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Newcastle na kujipatia bao la kusawazisha kunako dakika ya 56 likifungwa na Manquilo.

Man Utd walianza kulisakama lango la Newcastle na kufanikiwa kupata goli la pili kupitia tena kwa Ronaldo,Bruna Fernandes aliongeza la tatu dakika ya 80 kwa shuti kali kabla ya Jesse Lingard kukamilisha kalamu hiyo dakika ya 90+2 akiitumia vema pasi ya Paul Pogba.

banner

Hiyo ni mechi ya kwanza ya Ronaldo akirejea Old Trafford kwa mara ya pili akitokea Juventus.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited