Habari mbaya kwa Watanzania ni kwamba nahodha wa timu ya Taifa(Taifa stars) Mbwana Samatta atakosekana katika kikosi kitakachoivaa timu ya taifa ya Tunisia katika kuwania kufuzu Afcon mwakani.
Nahodha huyo anayeichezea klabu ya Fernabache ya nchini Uturuki atakosekana katika kikosi hicho kilichoweka kambi nchini Uturuki kutokana na kusumbuliwa na majeraha na hivyo madaktari kumshauri apumzike.
Taifa stars inatarajiwa kucheza na Tunisia ugenini mjini Tunis kisha kurudiana baada ya siku nne jijini Dar es salaam.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.