Home Soka Shikalo Uhakika Zesco

Shikalo Uhakika Zesco

by Sports Leo
0 comments

Sasa ni uhakika kuwa kipa mpya wa Yanga sc Farouk Shikalo atatumika katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Zesco baada ya shirikisho la soka barani Afrika (Caf) kutoka leseni ya kumtumia mchezaji huyo.

Kipa huyo aliyesajiliwa kutoka Bandari fc ya Kenya aliishia kuwa mtazamaji katika michezo miwili ya hatua ya awali ya michuano hiyo dhidi ya Township Rollers baada ya Caf kutokutoa leseni ya mchezaji huyo baada ya usajili wake kuchelewa kukamilika.

“Muda wowote kutoka sasa leseni ya Shikalo itawasili baada ya Caf kuruhusu atumike kwenye mechi inayokuja, lakini kwa Mustapha na Molinga wao bado na hatuwezi kuwatumia hadi tutakapofika makundi.Alisema kaimu katibu mkuu wa timu hiyo Dismas Ten.

banner

Kurejea kwa kipa huyo kumeipa nafuu klabu ya Yanga baada ya kuwa na makipa wawili Metacha Mnata na Kinda Ramadhani Kabwili hali iliyotia wasiwasi endapo mmoja ataumia.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited