Mabingwa wa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba sc wameibuka mabingwa wapya wa michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Azam fc 1-0 katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo uliomalizika muda mfupi uliopita.
Goli pekee la mchezo liliwekwa kimiani na mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda Meddie Kagere kwa mkwaju wa penati dakika ya 56 baada ya mlinda mlango Mathias Kigonya wa Azam kumfanyia madhambi winga Pape Ousmane Sakho.
Azam waliutawala fainali hiyo kwa kiasi kikubwa lakini hawakuweza kuweka mpira nyavuni licha ya kufanya mashambulizi mengi ya hatari langoni mwa Simba,ambapo mlinda mlango wa Aishi Manula alikuwa imara kuhakikisha nyavu zake haziguswi.
Winga kutoka Mali Pape Ousmane Sakho ameibuka mchezaji bora wa mashindano hayo huku Meddie Kagere akiibuka mfungaji bora kwa magoli matatu aliyofunga katika michuano hiyo,naye mlinda mlango Aishi Manula amekuwa golikipa bora wa mashindano hayo ya kusheherekea miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Huu unakuwa ubingwa wa nne wa Simba kwenye michuano hiyo na wanakuwa timu ya pili kuchukua kombe hilo nyuma ya Azam fc anayeongoza kwa kuchukua jumla ya makombe matano tangu mwak 2007.