Home Soka Simba ni Zaidi ya Tp Mazembe-Ajib

Simba ni Zaidi ya Tp Mazembe-Ajib

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba sc Ibrahim Ajib ameamua kutoa ufafanuzi kuhusu suala ya kutojiunga na timu ya Tp Mazembe ya kongo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kukipiga msimbazi.

Kiungo huyo aliyesajiliwa kutoka Yanga baada ya mkataba wake kuisha alisema ofa ya simba iliizidi ya Mazembe hivyo hakuna na namna zaidi ya kusaini baada ya wakongo hao kuweka dau dogo.

Ajibu ambaye aliondoka Simba miaka miwili iliyopita amedai pia licha maslahi makubwa aliyopewa na klabu hiyo pia aliondoka kwa amani licha ya kuwa alijiunga na mahasimu wakubwa wa klabu hiyo Yanga sc.

banner

Hivi karibuni wawakilishi wa Tp mazembe walitua nchini kuisaka saini ya mshambuliaji huyo bila mafanikio licha kuongeza dau mpaka kufikia dola elfu hamsini ambazo ni zaidi ya shilingi milioni mia za kitanzania.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited