Home Soka Simba Queen Watwaa Ngao ya Jamii

Simba Queen Watwaa Ngao ya Jamii

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya wanawake ya Simba Queens imefanikiwa  kubeba taji la kwanza la msimu huu wa ligi ya wanawake la Ngao ya Jamii 2023 kwa kuifunga JKT Queens mikwaju ya penalti 5-4 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya 1-1 mechi iliyopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Simba Queen imetwaa taji hilo la kwanza la ufunguzi wa msimu wakifuata nyayo za kaka zao Simba sc ambao walitwaa taji hilo mwanzoni mwa msimu huu katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga wakiifunga Yanga sc kwa matuta.

Licha ya kutanguliwa kufunga bao la mapema la dakika ya 14 likifungwa na Stumai Abdallah Simba Queen walijipanga na kufanya mashambulizi mazito yaliyozaa bao dakika ya 25 ya mchezo likifungwa na Danai Bhobho kutokana na kona ya Mwanahamis iliyozagaa langoni hapo na kumkuta mfungaji.

banner

Baada ya dakika tisini ya kawaida mwamuzi aliamuru mapigo ya penati tano ambapo Jkt Queens walipata nne huku Simba Queen wakipata tano.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited