Klabu ya Simba sc imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali michuano ya kombe la shirikisho nchini la Azam ambapo wamefuzu baada ya kuifunga klabu ya Dodoma Jiji Fc mabao 2-0 yaliyofungwa na nahodha John Boko.
Kutokana na ushindi huo hatua ya nusu fainali itazikutanisha timu za Simba sc na Azam Fc huku Yanga sc wakicheza na Biashara United ya mkoani mara huku michezo yote ikifanyika katika viwanja huru.
Mechi hiyo itakayo wakutanisha Simba sc dhidi ya Azam Fc ni kama mechi ya kisasi maana Azam Fc walikubali kipigo cha mabao 4 katika michuano kama hiyo msimu ulioisha hivyo hii ni Fursa kwao kuonyesha kwamba kipigp hicho kilikua ni bahati mbaya.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc mpaka sasa ndio timu bora hapa nchini hivyo kura za mashabiki wengi zimeangukia kwao kuwa wanaweza kutwaa mataji yote mawili mfululizo.