Home Soka Simba sc Waiweka El Merrekh Matatani

Simba sc Waiweka El Merrekh Matatani

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imeiripoti Klabu ya El Merreikh ya Sudan kwa Shirikisho la Soka Afrika “CAF” kwa kuwatumia Wachezaji ambao hawakustahili kucheza Mechi Kati ya Timu hizo Huko Khartoum Katika Raundi ya tatu ya Hatua ya Makundi ya Mashindano.

-Wachezaji, Ramadan Agab na Bakhit Khamis walicheza Mechi hiyo huku wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita waliyopewa na Chama cha Soka Sudan (SFA); Ushahidi wa barua zimepatikana, zinaonesha kuwa SFA iliwafungia wachezaji hao kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kusaini mikataba katika timu mbili tofauti kwa Wakati mmoja adhabu ambayo inaishia mwezi Aprili.

Katika Mchezo uliochezwa jijini Khartoum, Jumamosi iliyopita uliisha kwa Suluhu, Simba SC sasa huenda ikapata ushindi wa mezani dhidi ya Al Merrikh ambapo Ni magoli Mawili na Pointi tatu.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited