Klabu ya Simba sc imezindua applications ya mtandao inayosaidia upatikanaji wa taarifa mbalimbali za klabu hiyo huku kila mwanachama atakaejiunga atachangia kiasi cha shilingi elfu mbili kwa mwezi.
Applications hiyo itajulikana kama Simba App na inapatikana kwa njia zote za mifumo ya simu yaani AppStore na Playstore huku ikitarajiwa kuingiza mapato ya kutosha kwa klabu hiyo kutokana na kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za klabu.
Aidha wazo la klabu za ligi kuu nchini kuwa na huduma hiyo ilizinduliwa na Dismas Ten aliyekua afisa habari wa klabu ya Yanga sc ambapo akiwa katika klabu ya Mbeya City alianzisha wazo hilo na alilileta Yanga sc ambao kwa msimu uliopita waliingiza takribani milioni 240 za kitanzania.