Home Soka Simba Sc Yafunga Usajili na Mastraika Wawili

Simba Sc Yafunga Usajili na Mastraika Wawili

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imefunga usajili wa dirisha dogo la usajili baada ya kukamlisha usajili wa washambuliaji wawili kuja kuongeza nguvu klabuni hupo wakitokea nchi za Ivory Coast na Gambia kuja kukamilisha safu ya kutetea ubingwa klabuni hapo.

Staa wa kwanza kusajiliwa klabuni hapo siku ya mwisho ya kufunga usajili ni Pa Omar Jobe raia wa Gambia ambaye alikua anaichezea klabu ya Zhenis ya nchini Kazakhstan ambayo aliichezea jumla ya michezo 25 na kufunga mabao 13.

banner

Staa wa pili kufunga usajili klabuni hapo ni Freddy Michael Kouablan raia wa Ivory Coast mwenye miaka 26 ambaye amesainiwa kwa miaka miwili akitokea klabu ya Ligi kuu ya Zambia ya Green Eagles.

Usajili wa Freddy umeonekana kuwa gumzo kutokana na kuwa anafanya vizuri huku akinunuliwa kutoka klabu hiyo ya Zambia ambapo mpaka muda huu ligi ikiwa inaendelea amefanikiwa kuongoza katika safu ya ufungaji akiwa na mabao 14 na pasi za magoli 4.

Simba sc imewasajili wachezaji ikiwa ni pendekezo la kocha Benchika ambaye alikua anahitaji washambuliaji wa haraka ambao watakuja kuingia kikosi cha kwanza moja kwa moja.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited