Klabu ya Simba imesaini mktaba wa miaka miwili na shirika la ndege nchini(ATCL) kushirikiana katika maswala mbalimbali ya usafiri pindi timu hiyo itakapokuwa inasafiri ndani na nje ya nchi.
Katika mkabana huo ATC ndio watakaokuwa na dhamana ya kuisafirisha Simba kwnye mashindano ya kimataifa,pia wanachama na mashabiki wa timu hiyo watanufaika kwa kupata nafasi ya kusafiri natimu hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez amesema kuwa ”thamani ya mkataba huu ni zaidi ya milioni 400,wanachama na mashabiki wetu watapata tiketi za bure,watapata punguzo pamoja na kupewa kipaumbele pindi watakapokuwa na safari”.
Naye Mkurugenzi wa ATCL Injinia Ladislaus Matindi Simba watasaidia kuitangaza Air Tanzania kupitia safari zao katika mashindano ya kimataifa,pia timu ya wanawake ya Simba watavaa nembo ya Air Tanzania mbele ya jezi zao.Na upande wa Simba watapata fedha pamoja na faida nyingine.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.