Home Soka Simba sc Yaishusha Daraja Ruvu Shooting

Simba sc Yaishusha Daraja Ruvu Shooting

by Sports Leo
0 comments

Kufuatia kuifunga kwa mabao 3-0 klabu ya Simba sc imezamisha moja kwa moja jahazi la timu ya Ruvu Shooting kufuatia kushindwa kupata alama tatu katika mchezo huo huku ikiwa mkiani mwa msimamo wa ligi kuu nchini.

Kutokana na matokeo hayo imethibitika moja kwa moja kuwa Ruvu shootinga wameshuka daraja licha ya kuwa na michezo miwili mkononi wakiwa na alama 20 pekee katika michezo 28 ya ligi kuu nchini waliyocheza mpaka sasa.

Katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Complex Dar es salaam mabao ya Simba sc yalifungwa na Cletous Chama dakika ya 30 huku Pape Osmane Sakho akifunga mabao mawili dakika za 72 na 90+3.

banner

Simba sc sasa imefikisha alama 68 ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini huku tayari Yanga sc ikiwa imefanikiwa kutwa ubingwa wa ligi kuu nchini kwa mara ya 29.

Ruvu shooting wameshuka daraja huku Polisi Tanzania nayo ikiwa hatarini kushuka daraja ambapo italazimika kushinda michezo yake mitatu iliyosalia huku ikiziombea mabaya Mtibwa Sugar na Kmc zilizo juu yake katika msimamo wa ligi kuu nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited