Home Soka Simba Sc Yamnasa Balua

Simba Sc Yamnasa Balua

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Simba Sc imemtambulisha mchezaji Edwin Balua kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo ikimsajili kutoka klabu ya Tanzania Prisons inayoshiriki ligi kuu ya Nbc nchini Tanzania.

Balua mwenye uwezo wa kucheza nafasi za kiungo wa juu na mshambuliaji namba mbili huku pia akiwa na uwezo wa kucheza nafasi zote za winga anajiunga na klabu hiyo kuja kulete changamoto kwa Ladack Chasambi,Willy Onana,Luis Miqqiuson,Karabaka na wengine ambao wanacheza eneo hilo.

Balua ametambulishwa rasmi siku ya jumatano mchana kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ambapo taarifa rasmi ilisomeka kuwa “Karibu Simba SC, Edwin Balua.” ambapo ilizua maoni mbalimbali ya mashabiki wa klabu hiyo.

banner

Kocha Abelhack Bechika amekua akifanya mageuzi makubwa kikosini akisajili mastaa wa maana kuja kuongeza nguvu huku akiwatema baadhi kutokana na viwango vyao kushuka.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited