Home Soka Simba Sc Yapaa Kuifuata Wydad

Simba Sc Yapaa Kuifuata Wydad

by Sports Leo
0 comments

Kikosi cha Simba sc mchana wa leo kimeanza safari  kutoka Dar es Salaam kuelekea nchini Morocco kwaajili ya maandalizi ya mechi ya tatu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca itakayofanyika siku ya Jumamosi Desemba 9 katika Uwanja wa Mohamed V saa 4:00 usiku.

Msafara wa kikosi hicho umeanza safari mapema mchana wa leo kwenda kupambania alama tatu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo fainali kupitia kundi B lenye timu za Jwaneng Galaxy,Asec Mimosas na Wydad Athletics club.

Hata hivyo safari hiyo ya zaidi ya masaa matano ambayo itailazimu Simba kupanda ndege mbili hadi tatu tofauti ni ya kimkakati zaidi ambapo kocha mkuu mpya wa kikosi hicho, Mualgeria Abdelhak Benchikha ndiye amependekeza timu kuwahi ili ijiandae na walau kwa siku mbili.

banner

Pia kocha huyo ameondoka na takribani mastaa wake wote wa kikosi cha kwanza kilichosafiri katika mchezo uliopita dhidi ya Galaxy ambapo kilipata suluhu na kufikisha alama mbili katika kundi B huku ikiwa haina cha kufanya zaidi ya kupata alama tatu katika mchezo huo.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited