Klabu ya Simba sc imewasili nchini Zimbabwe kuelekea mchezo wa kufuzu michuano ya klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Fc Platnum ya nchini humo utakaofanyika siku ya Jumatano.
Simba sc imewasili mapema baada ya awali kumtanguliza mtendaji mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez huku pia baadhi ya wajumbe wakitangulia kuandaa mazingira mazuri ili kupata ushindi.
Simba sc imeingia katika hatua ya pili ya mtoano baada ya kuwatoa Plateau United ya nchini Nigeria na endapo watafuzu watajikatia tiketi ya kuingia hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.