Home Soka Sina Mkataba na Apr-Bigirimana

Sina Mkataba na Apr-Bigirimana

by Sports Leo
0 comments

Mshambualiji mpya wa klabu ya Yanga Issa Bigirimana amekana kuwa na mkataba na klabu ya Apr ya Rwanda baada ya waajiri wake hao kutoa taarifa ya kuwa na mkataba na mshambualiaji huyo.

Bigirimana mwenye uraia wa Burundi hivi sasa anaichezea Apr ambapo mkataba wake na wanajeshi hao unaisha msimu huu hivyo kuwa na uhuru wa kuchangua wapi akachezee kwa mujibu wa sheria za Fifa zinazomruhusu mchezaji mwenye mkataba wa chini ya miezi sita kuingia katika mazungumzo na klabu yeyote na hata kusaini mkataba wa awali.

Katika taarifa ilyotolewa na katibu mkuu wa klabu ya Apr Adolphe kalisa alidai kuwa klabu hiyo ina mkataba na Bigirimana mpaka mwaka 2020 na kuitaka kjlabu ya Yanga ifate taratibu za usajili.Bigirimana amekanusha taarifa hiyo na kusisitiza kuwa yeye ni mchezaji huru na atajiunga na yanga baada ya kufikia makubaliano na klabu hiyo ya jangwani.

banner

“Awali ilikua nisaini Apr lakini nilisubiri mazungumzo yangu na Yanga nione yatafikia wapi na baada ya kuwa tumeshakubaliana nikasaini kujiunga nao na mkataba wangu na Apr unaisha msimu huu na hata Ferwafa(shirikisho la soka la Rwanda) wanafahamu hilo kwani nakala halisi ya mkataba wanayo hivyo Yanga wasihofu kuhusu hilo”.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited