Klabu ya Singida Fountain Gates imekamikisha Usajili wa Mlinzi wa kushoto raia wa Botswana Benson Kitso Mangolo kuja kuongeza nguvu katika eneo hilo ambalo mpaka sasa anacheza Gadiel Michael na Yahaya Mbegu kikosini humo.
Benson ambaye amewahi kuwa mchezaji bora wa mwaka nchini Botswana, kabla ya kukamisha usajili wake na matajiri wa Alizeti wenye makazi yao mkoani Singida huku ikifahamika kuwa Benson alikuwa ameshaitumikia klabu ya Jwaneng Galaxy inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika,
Usajili umefanikishwa kwa kiasi kikubwa na Olebile Sikwane ambaye ni Mtendaji mkuu (CEO) wa klabu hiyo ya Singida ambapo kutokana na kufanya kazi nchini humo ilikua rahisi kwake kukamilisha Usajili huo haraka zaidi,
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Singida FG katika usajili huo wameishinda Changamoto kutoka Kwa baadhi ya Vilabu kutoka Afrika Kusini ikiwemo Amazulu Fc ambayo ilikua ikimnyemelea kwa ukaribu zaidi.