Beki wa mabingwa wa kihistoria Yanga, Paulo Godfrey Boxer leo ameanza mazoezi mepesi tayari kwa mapambano.
Boxer aliumia kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambao ulipigwa August 10 kwenye uwanja wa Taifa
Alitonesha majeraha hayo ya nyama za paja katika mchezo wa marudiano uliopigwa nchini Botswana August 24
Msomaji wa Yanga News Blog: Boxer amesema amekuwa akipatiwa tiba nzuri na matarajio yake atarudi uwanja siku sio nyingi
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Namshukuru Mwenye ez Mungu sasa ivi naendelea vizuri na matibabu na nimeshaanza mazoezi mepesi. Natibiwa kwenye Hospitali ya Dk Maliali. Sasa ivi niko vizuri na mazoezi nimeshaanza,” amesema
“Niwajulishe wadau wa soka na mashabiki wa Yanga kuwa mimi sitibiwi Manzese kama watu wanavyoongea, natibiwa kwa Dk Maliali, niko vizuri siku sio nyingi nitarudi uwanjani”